Viongozi wa Ulaya kufanya mazungumzo kabla Trump na Zelensky
17 Agosti 2025Matangazo
Ushawishi huo una lengo la kutoa mwelekeo wa kile wanachotaka kifanyike au kitekelezwe. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer, na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz wanatarajiwa kufanya mkutano kwa njia ya video wa kile kinachoitwa "Muungano wa Wenye Nia" saa tisa alasiri. Muungano huo ni kundi lisilo rasmi la mataifa yanayoiunga mkono serikali ya Kyiv dhidi ya uvamizi kamili wa Urusi ulioanzishwa Februari 2022. Mazungumzo hayo yanakuja baada ya mkutano wa hali ya juu uliofanyika Ijumaa huko Alaska kati ya Trump na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Licha ya Trump kumpokea vyema kiongozi wa Kremlin, mkutano huo haukuleta mafanikio yoyote ya kusitisha vita.