Viongozi wa Ulaya kujadili hatma ya ulinzi wa kikanda
3 Februari 2025Matangazo
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami NATO, Mark Rutte na Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer watajiunga na viongozi hao kwa majadiliano ya namna ya kuimarisha uwezo wa ulinzi barani Ulaya.
Kwa miaka kadhaa sasa, Ulaya imekuwa inahangaika kuongeza uzalishaji wa silaha na vita vya Urusi nchini Ukraine vimezidisha wasiwasi juu ya hali ya usalama ya kanda hiyo mnamo siku za usoni.
Soma pia:Denmark na Ujerumani zataka Ulaya iliyo thabiti zaidi kukabiliana na vitisho
Viongozi wanaokutana leo watatafakari uwezekano wa kufadhili miradi zaidi ya ulinzi kupitia Benki ya Uwekezaji ya Ulaya baada ya mapendekezo ya kutumia mikopo ya serikali kukosa uungwaji mkono wa kutosha.