Viongozi wa Ulaya kujadili bajeti za ulinzi na Ukraine
6 Machi 2025Mkutano huo unalenga kuidhinisha hatua nzito za kuongeza matumizi kwenye sekta ya ulinzi na kutoa ahadi ya kuendelea kuisaidia Ukraine baada ya Marekani kuisitishia kwa muda misaada ya kijeshi.
Viongozi hao wa nchi 27 wanachama wa umoja huo watajiunga na mwenzao wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kwenye mkutano unaofanyika chini ya kiwingu cha mashaka ya kulegalega kwa mahusiano kati ya mataifa ya Ulaya na Marekani.
Nchi za Ulaya zina wasiwasi kwamba Urusi iliyoivamia Ukraine miaka mitatu iliyopita inaweza kuishambulia nchi nyingine ya bara hilo na Marekani iliyo mshirika wa siku nyingi haitojotokeza kusaidia.
Kuelekea mkutano huo wa leo, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ametoa hotuba kwa taifa lake iliyowaambia pia viongozi wa Ulaya kuwa Urusi ni "kitisho kikubwa kwa bara hilo na Ulaya inayo jukumu la kuamua kuhusu hatma yake."
Hata hivyo mkutano huo wa leo tayari umeingia doa baada Hungary kukataa kuridhia tamko la pamoja la kuiunga mkono Ukraine.