SiasaAsia
Viongozi wa Thailand, Cambodia kukutana Malaysia
28 Julai 2025Matangazo
Idadi ya watu waliokwishauawa tangu mapigano hayo kuanza siku ya Alkhamis imefikia 30, wakiwemo raia 13 nchini Thailand na wanane nchini Cambodia, wakati mamlaka zikiripoti kwamba zaidi ya watu 200,000 wamehamishwa kutoka maeneo ya mpakani.
Hapo jana, Rais Donald Trump wa Marekani alisema anaamini Thailand na Cambodia zinataka kumaliza tafauti zao, baada ya kuwaambia viongozi wa nchi hizo kuwa hatahitimisha makubaliano ya kibiashara nao bila ya kwanza kuacha vita.
Hivi leo, waziri wake wa mambo ya kigeni, Marco Rubio, amesema maafisa wa Marekani wako nchini Malaysia kusaidia kwenye mazungumzo ya kuzipatanisha Thailand na Cambodia.