Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar wametia saini makubaliano ya kusitisha mapigano nchini humo katika kipindi cha saa 72 zijazo, hivyo kufufua matumaini ya kupatikana muafaka wa kuvimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan Kusini ambavyo vimedumu kwa miaka mitano na kusababisha vifo vya maelfu ya watu na mamilioni ya wengine kuachwa bila ya makazi.