Viongozi wa nchi za NATO wakutana The Hague
24 Juni 2025Viongozi wa nchi wanachama wa NATO wanakutana mjini The Hague katika mkutano wa kilele wa siku mbili, wenye lengo la kuonesha mshikamano wa kijeshi dhidi ya Urusi.
Licha ya kauli za awali za Rais wa Marekani Donald Trump za kuukosoa mfungamano huo, mkutano huu nchini Uholanzi unalenga kuimarisha ulinzi wa pamoja kwa kuongeza bajeti ya kijeshi. Trump anatarajiwa kushiriki mkutano huo kesho, Jumatano.
Katibu Mkuu waNATO, Mark Rutte, amesema jumuiya hiyo haiwezi kuendelea kuwa dhaifu mbele ya Urusi na inapaswa kuchukua hatua zaidi kuimarisha uwezo wake wa kiulinzi.
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ambaye mzozo wa nchi yake na Urusi ni ajenda kuu, ametaka NATO kuongeza uwekezaji katika uzalishaji wa silaha ndani ya Ukraine na kuzuia vipuri kutoka nje vinavyotumiwa na Urusi kutengeneza silaha.