Mataifa ya kiarabu kutowa mpango wao kuhusu Gaza
20 Februari 2025Matangazo
Nchi za Kiarabu zimeungana kuiunga mkono Gaza japo bado zimegawika kuhusu nani anapaswa miongoni mwao kulisimamia eneo hilo lililoharibiwa kwa vita na namna ya kufadhili ujenzi mpya wa eneo hilo.
Soma pia:Emirati yapinga kuhamishwa kwa Wapalestina Gaza
Mfalme Abdullah wa Pili wa Jordan amesema kwamba Misri ndiyo itakayowasilisha mpango wa hatua za kuchukuliwa katika kusimamia mustakabali wa Gaza.