Viongozi wa Marekani, EU na Ukraine kukutana mjini Paris
17 Aprili 2025Matangazo
Mkutano huo utahudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio, mjumbe maalumu wa Rais Donald Trump , Steve Witkoff, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na waziri wake wa mambo ya nje Jean-Noel Barrot. Viongozi hao wanatarajia pia kujadili mzozo wa Mashariki ya Kati.
Ukraine itawakilishwa na waziri wake wa mambo ya nje Andrii Sybiha pamoja na mkuu wa ofisi ya Rais Andriy Yermak ambaye amesema watakutana pia kwa mazungumzo na viongozi wa Ujerumani na Uingereza kuhusu suala la dhamana ya usalama ikiwa kutafikiwa mpango wa amani.