MigogoroMashariki ya Kati
Kundi la G7 lataka mivutano ipungue Mashariki ya Kati
17 Juni 2025Matangazo
Tamko hilo la pamoja la Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani limesema Israel ina haki ya kujilinda na limesisitiza pia umuhimu wa kuwalinda raia wakati mashambulizi kati ya Iran na Israel yakiwauwa raia wa pande zote mbili.
Soma zaidi: Netanyahu: Tutabadili sura ya Mashariki ya Kati
Mbali na kauli hiyo, viongozi wa nchi hizo wameweka wazi msimamo wao kuwa, Iran haiwezi kumiliki silaha za nyuklia. Mkutano huo wa G7 uliitishwa kwa madhumuni ya kusaidia kutatua changamoto kadhaa lakini umeishia kugubikwa na mzozo kati ya Israel na Iran baada ya Israel kuanzisha mashambulizi dhidi ya Iran Ijumaa iliyopita.