SiasaUrusi
Viongozi wa China, Urusi na Korea Kaskazini kukutana Beijing
2 Septemba 2025Matangazo
Putin, ambaye kwa sasa yuko ziarani nchini China, anatarajiwa kuhudhuria gwaride la kijeshi hapo kesho na mwenyeji wake, Rais Xi Jinping , katika sherehe za kuadhimisha miaka 80 tangu vimalizike Vita vya Pili vya Dunia.
Aidha, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, atahudhuria pia gwaride hilo na anatazamiwa pembezoni mwa maadhimisho hayo kufanya mazungumzo na Putin.
China, Urusi na washirika wao, wanajaribu kubadili utaratibu wa uendeshaji ulimwengu unaosimamiwa na Marekani na mataifa ya Magharibi.