Viongozi wa chama cha Kabila kuhojiwa mahakama ya kijeshi
10 Machi 2025Mwanasheria wa viongozi na mshauri wa zamani wa masuala ya ulinzi wa kabila Jean Mbuyu amesema sababu hasa za wito huo hazijawekwa wazi lakini Rais Felix Tshisekedi alimshtumu Kabila hivi karibuni kuwafadhili waasi wa M23 ambao wameteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Kongo.
Soma zaidi:Mashambulizi ya ADF yasababisha mauaji ya watu 9 Kongo
Mbuyu amesema ofisi ya mwendesha mashtaka wa kijeshi ilituma barua kumi kwa wanachama wa Chama cha Kabila cha People's Party for Reconstruction and Democracy ingawa ni watu watatu tu ndio wanaotarajiwa kujitokeza kwa mahojiano katika mjini Kinshasa.
Rwanda inakanusha kutoa silaha na wanajeshi kwa M23, na inasema kwamba vikosi vyake vinafanya kazi ya kujilinda dhidi ya jeshi la Kongo na wanamgambo wanaoichukia Rwanda.