Viongozi wa Afrika kujaidli ulipaji fidia wa zama za utumwa
13 Februari 2025Matangazo
Hata hivyo, wanaweza kutarajia upinzani kutoka kwa watawala wao wa zamani, ambapo wengi wao wamefuta uwezekano wa kuyarekebisha maovu hayo ya kihistoria.
Kwenye mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, viongozi wanapanga kuwa na mpango wa kile wanachosema ni maono ya pamoja ya jinsi fidia zinavyopaswa kuwa, kuanzia fidia ya kifedha na kukiri rasmi makosa ya zamani hadi mageuzi ya sera.
Hilo limethibitishwa na baraza la kiuchumi, kijamii na kiutamaduni la Umoja wa Afrika. Kuanzia Karne ya 15 hadi 19, karibu Waafrika milioni 12.5 walitekwa, wakasafirishwa kwa nguvu na hasa wafanyabiashara wa Ulaya na kuuzwa kama watumwa.