Viongozi wawasili Moscow kuhudhuria "sherehe za ushindi"
8 Mei 2025Matangazo
Baadhi ya viongozi hao ni kutoka China, Brazil, Vietnam, Venezuela, Cuba, Laos, Mongolia, Misri, Armenia, Azerbaijan, Kazakhstan, Slovania, Belarus, Myanmar, Burkina Faso, Zimbabwe, Jamhuri ya Congo, Ethiopia na Guinea ya Ikweta. Gwaride la kijeshi litafanyika kesho Ijumaa mjini Moscow.
Ulaya pia imeadhimisha sherehe hiyo ya miaka 80 tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia, huku viongozi wa kisiasa wakikitaja kipindi hicho kama mwanzo wa amani isiyo na mfano barani humo lakini ikiadhimishwa chini ya kiwingu cha uvamizi wa Urusi chini Ukraine.