Viongozi mbalimbali waomboleza kifo cha Sam Nujoma
10 Februari 2025Matangazo
Salaam za pole zimeendelea kumiminika kufuatia kifo cha cha rais wa kwanza wa Namibia Sam Nujoma ambaye pia anatambuliwa kuwa baba wa taifa hilo. Sam Nujoma, ambaye aliongoza vita vya miongo mitatu vya kupigania uhuru wa Namibia kutoka kwa utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amemtaja Nujoma kwamba alikuwa na msukumo mkubwa katika mapambano ya ukombozi wa nchi yake dhidi ya utawala wa wazungu wachache.
Mfalme Charles wa Uingereza ni miongoni mwa viongozi walioomboleza kifo cha Nujoma, akimwelezea kama mtu aliyekuwa na dhamira ya maisha ya uhuru na demokrasia na kwamba mchango wake katika historia ni mkubwa.