Viongozi kadhaa wa upinzani wakamatwa Uturuki
8 Julai 2025Wizara hiyo imeutangaza uamuzi wa kumfukuza Böcek na mameya wengine wawili waliokamatwa mwishoni mwa juma. Kulingana na polisi, meya huyo pia anashikiliwa kwa mahojiano kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili. Wakati huo huo, Mwendesha mashtaka nchini Uturuki ameamuru kukamatwa kwa mwenyekiti wa chama kikuu cha Upinzani cha Republic People's Party (CHP) mjini Istanbul Ozgur Celik. Kukamatwa kwa Celik kumetajwa kama sehemu ya uchunguzi kuhusiana na uchaguzi wa ndani wa chama hicho. Chama kikuu cha upinzani cha Uturuki CHP kinakabiliwa na shinikizo la mahakama huku mameya wake wasiopungua 15 wakiwa gerezani kabla ya kesi kusikilizwa akiwemo meya maarufu wa Istanbul Ekrem Imamoglu aliyeondolewa mamlakani. Upinzani nchini humo unauona mwenendo huo kuwa unachochewa kisiasa.