Vikosi vya Ukraine vyakaribia kuzingirwa ndani ya Urusi
8 Machi 2025Tathmini ya shirika la habari la Reuters iliyochambua taarifa za kijeshi inaonesha nafasi ya Ukraine kwenye mapigano ya mkoa wa Kursk imebadilika ndani ya siku tatu zilizopita baada ya Moscow kutanua kampeni yake ya kuvikabili vikosi vya Ukraine.
Inaarifiwa kwamba operesheni hiyo ya Urusi inakaribia kukigawa sehemu mbili kikosi cha wanajeshi wa Ukraine na kuziba njia za kuwafikishia wapiganaji wake mahitaji.
Taarifa hizo ni pigo kwa Ukraine iliyotumai kuwauwepo wa wanajeshi wake ndani ya ardhi ya Urusi ungeisaidia kuwa na usemi fulani kwenye meza ya mazungumzo ya kusaka amani kati yake na Moscow.
Hali hiyo inashuhudiwa katika wakati Marekani iliyokuwa mshirika wa karibu wa nchi hiyo imesitisha kuipatia Ukraine taarifa za kiintelejinsia na imeongeza shinikizo la kuitaka kutafuta mkataba wa amani na Urusi.