VIKOSI VYA KIJAPANI KUSAIDIA IRAQ:
10 Desemba 2003Matangazo
TOKYO: Ujapani imeamua kuwapeleka wanajeshi wake nchini Iraq.Waziri mkuu Junichiro Koizumi ameutetea uamuzi huo akisema kuwa ni wajibu wa Ujapani kuisaidia Marekani kuijenga Iraq.Kiasi ya wanajeshi 600 watasaidia katika ujenzi wa barabara na watashughulika na huduma za misaada ya kiutu.Tangu kumalizika Vita Vikuu vya pili jeshi la Ujapani halijapigana vita.Katiba ya nchi hiyo hairuhusu vikosi vya kupigana vita-ni vikosi vya ulinzi tu vinavyoruhusiwa nchini Ujapani.