Vikosi vya Israel vyaongeza mashambulizi Gaza
14 Agosti 2025Kwa mujibu wa wakazi na wahudumu wa afya watu wanane waliuawa baada ya Israel kulenga nyumba katika mtaa wa Zeitoun, huku mtu mmoja akiuawa katika shambulio la anga kwenye jengo lililoko kwenye kitongoji cha Shejaia. Wengine wawili waliuawa katika mashambulizi ya mizinga katika mtaa wa Tuffah, sehemu nyingine ya Jiji la Gaza.
Katika juhudi za kuzuia kuongezeka kwa mashambulizi, Misri imekuwa mwenyeji wa ujumbe wa Hamas unaoongozwa na mpatanishi mkuu Khalil Al-Hayya, ambaye amesema Hamas iko tayari kurejea kwenye mazungumzo ya kusitisha mapigano na kujadili makubaliano ya kumaliza vita.
Hata hivyo pengo kati ya pande Israelna Hamas linaonekana kuwa bado ni kubwa kuhusu masuala muhimu, ikiwemo kiwango cha kujiondoa kwa kijeshi la Israel na madai ya kuitaka Hamas isalimishe silaha zake.