MigogoroPakistan
India na Pakistan yashambuliana katika jimbo la Kashmir
27 Aprili 2025Matangazo
Haya yamesemwa leo na maafisa wa India, wakati uhusiano kati ya mataifa hayo mawili pinzani yenye uwezo mkubwa wa nyuklia ukizorota zaidi katika kipindi cha miaka kadhaa.
Jeshi la India limesema leo kuwa kumekuwa na visa vya ufyatuaji risasi ambavyo havikuchochewa kutoka upande wa Pakistan katika eneo la mpaka unaozitenganisha nchi hizo mbili.
Soma zaidi: Pakistan yazifungia ndege za India anga yake
Jeshi hilo limeongeza kuwa wanajeshi wake walijibu shambulizi hilo kwa silaha nyepesi.
Hata hivyo Pakistan haijathibitisha tukio hilo la hivi karibuni la ufyatulianaji risasi.
Wizara ya mambo ya ndani ya India imekabidhi uchunguzi kuhusu shambulizi hilo kwa Shirika la Kitaifa la Ujasusi, ambalo pia linahusika na kukabiliana na ugaidi.