Kumekuwepo na mabadiliko makubwa kwenye mitindo ya uvaaji kote ulimwenguni. Katika nyakati hizi huwezi kushangaa kumuona msichana amevaa pengine raba ambazo pia anavaa mwanaume, na kwa upande wa wanaume pia huwa ni hivyohivyo. Je, nini kimesababisha hali hii, na je wewe ni mmoja wapo? Karibu usikilize makala hii ya Vijana Mchakamchaka, usikie wenzako wanasemaje?