Vifo vya wagombea 17 nchini Ujerumani vyazua minong'ono
4 Septemba 2025Hivi leo kiongozi wa chama mbadala kwa Ujerumani cha AfD katika jimbo la North Rhine Westphalia amesema chama chake hakina ushahidi kwamba vifo vya wagombea wake vimesababishwa na hali isiyokuwa ya kawaida.
Jimbo la North Rhine Westphalia linajiandaa kuingia kwenye uchaguzi wa, wilaya,manispaa na serikali za mitaa Septemba 14 lakini kampeni za uchaguzi huo zimeingia doa.
Katika kipindi cha siku kadhaa sasa kampeini zimegubikwa na taarifa za vifo vya wagombea huku kiongozi mwenza wa chama cha AfD Alice Weidel na bilionea maarufu Elon Musk anayekiunga mkono chama hicho wakilizungumzia suala hilo kwenye mtandao wa X.
Hata hivyo ametaja kwamba minong'ono iliyoenea kwenye mitandao inaakisi hali halisi ya namna ambavyo mamlaka za Ujerumani inakitazama chama hicho ambacho kiko kwenye uchunguzi wa idara za ujasusi, kama chama kinachoshukiwa kuwa cha itikadi kali za siasa za mrengo wa kulia katika ngazi ya kitaifa. Kwa mujibu wa data rasmi wagombea 16 wamekufa wakati wa kampeini za uchaguzi huu ujao kwenye jimbo la North Rhine Westphalia ambapo saba ni wa chama hicho cha AfD.
Vincentz amesema, hata ikiwa hivi sasa kwa wengi yanafikiriwa kama ni mauaji ya kisiasa ni kwasababu hii ni athari ya moja kwa moja ya vita vya mara kwa mara inavyopigwa chama cha AfD kwa miaka.
AfD kinatafsiriwa kama chama mbadala kwa Ujerumani
AfD ni chama kikuu cha Upinzani hivi sasa kikishikilia zaidi ya asilimia 20 ya kura za uchaguzi wa bunge kitaifa uliofanyika mwezi Februari.
Wagombea wake saba wamekufa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaokuja kati ya wagombea jumla 16 waliokufa NRW. Katika visa vinne ambavyo vimeshachunguzwa, polisi tayari imeshafuta uwezekano kwamba ni mauaji.
Ingawa hakuna chama kingine chochote ambacho kimeshuhudia kufiwa na zaidi ya mgombea mmoja. Kifo cha mgombea kwenye uchaguzi nchini Ujerumani kinaweza kusababisha mamlaka kulazimika kuchapisha upya karatasi za kupiga kura au hata kuandaa uchaguzi maalum ambao, wakati mwingine unaweza kufanyika siku hiyo hiyo ya uchaguzi.
Msemaji wa tume ya uchaguzi ya jimbo la NRW awali alijaribu kutuliza mihemko iliyoongezeka mitandaoni kuhusu vifo hivyo vya wagombea akiliambia shirika la habari la Dpa kwamba sio jambo geni kwa wagombea kufa kipindi cha Kampeni. Uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita uliofanyika katika jimbo hili la NRW mnamo mwaka 2020 viti 20,000 viligombewa