Haki za watoto katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinakabiliwa na changamoto si haba. Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia watoto, watoto 6,200 wamekufa DRC kutokana na surua na wengine 17,000 kutokana na maradhi mengine katika mwaka mmoja. Makala ya Mbiu ya Mnyonge inawaangazia watoto wasiopewa tiba ambayo ni haki ya msingi. Msimulizi ni Saleh MWanamilongo.