Vifo kutokana na mvua kubwa Korea Kusini vyafikia 17
21 Julai 2025Matangazo
Mvua kubwa nchini Korea Kusini zimesababisha vifo vya watu wasiopungua 17 katika siku chache zilizopita huku watu 11 wakiwa hawajulikani waliko. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu rasmi za serikali ya Korea Kusini.
Nchi hiyo kwa kawaida hukumbwa na mvua nyingi mwezi Julai na huwa imejiandaa vyema lakini wiki hii maeneo ya kusini mwa nchi yalikumbwa na mvua nyingi kabisa kwa saa kuwahi kurekodiwa.
Kulikuwa pia maporomoko hatari ya tope upande wa kaskazini mapema jana Jumapili, huku karibi milimita 170 za nmvua zikirekodiwa katika kaunti ya Gapyeong katika mkoa wa Gyeonggi, mashariki mwa mji mkuu Seoul, yaliyosababisha vifo vya watu kiasi wawili na watano hawajulikani waliko.