Vifo katika mripuko mjini Kerbala, Iraq
27 Desemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Nchini Iraq, mji wa Kerbal umetikiswa na orodha ya miripuko. Watu si chini ya wanne wameuawa na wengine 60 wamajeruhiwa katika mashambulio hayo, waliarifu wanajeshi wa Kipoland waliousimamia mjini wa Kerbala. Inasemekana nao wanajeshi wa kigeni ni miongoni mwa watu waliouawa. Yamefanyika orodha ya mashambulio ya makombora ya mkono karibu ya makao makuu ya wanajeshi wa mwungano mjini Kerbala, alisema msemaji wa wanajeshi wa Poland. Mbali na vituo vya kijeshi, inasemekana vimeshambuliwa pia vituo katika chuo kikuu, manispaa na jengo la polisi.- Na katika mji wa Iraq ya Kaskazini, Mossul, wanajeshi washika zamu wa Kimarekani wamewauwa Wairaq wanne katika mashambuliano ya silaha. Msemaji wa Kimarekani alisema wanajeshi wao walishambuliwa kwa makombora ya mkono kutokea gari lililopita njia na washambuliaji hao waliuawa katika operesheni ya msako iliyofuatia muda tu baadaye.