Vifo kadha katika shambulio Iraq:
14 Februari 2004BAGHDAD:
Nchini Iraq wameuawa watu 20 na kujeruhiwa
zaidi ya 35 watu wasiojulikana
walipokishambulia kituo cha polisi mjini
Falluja, wameripoti madakitari. Wafungwa miya
kadha walitumia mashambuliano hayo yaliyodumu
muda mrefu kukimbia. Mjini Washington Waziri wa
Mambo ya Ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld
amefafanua tena kwamba hata kama Marekani ina
niya ya kuikabidhi Iraq madaraka yake hapo Juni
30, lakini haina maana kuwa tarahe hiyo
itahamisha wanajeshi wake kutoka Iraq. Bwana
Rumsfeld alisema haikuwekwa bado tarehe ya
kuhamishwa wanajeshi wa Kimarekani. Pia
hapawezi kufanywa uchaguzi wa moja kwa moja
kabla ya tarehe hiyo alidokeza mjumbe wa UM kwa
Iraq, Lakhdar Brahimi baada ya mazungumzo yake
pamoja na kiongozi Kishiya wa Iraq, Ayatollah
Ali Sistani.